![]() |
Wajasiriamali wamejikuta katika matatizo ya kubeba mizigo ya madeni kiasi cha kushindwa kuendelea |
Nini maana ya mtaji?
Watu wengi wanaufahamu "Mtaji" kwa lugha rahisi kama "Kianzio" cha biashara. Ni kweli, kwa mfano mtaji wa mama Ntilie ni Maji, sufuria, jiko, mkaa, mwiko, sahani, pamoja na fedha ya kununulia chakula kama mchele, nyanya, maharage, chumvi n.k.
Sasa basi katika mtiririko wa mahitaji yaliyotajwa hapo, vyote vinahitaji pesa ili kuvipata.
Tatizo liko wapi?
Kupata mtaji kwa nyakati hizi imekuwa jambo linalosumbua watu wengi. Mabenki yanasita kukopesha wafanya biashara wadogo sana (Micro businesses) kutokana na sababu kadha wa kadha ambazo kwayo ukiangalia zina uzito. Kada hii ya wafanya biashara huwa hawaaminiki kwa wakopaji wakubwa kama mabenki na taasisi za fedha kutokana na sababu zifuatazo: Hawana ofisi za kudumu; Wanakosa dhamana n.k
Kupata fedha za kuanzisha biashara imekuwa ni kama ndoto!!
Suala la upatikanaji wa mtaji
umeelezwa na wajasiriamali wengi kuwa kikwazo kikubwa na kinachozuia
wajasiriamali wapya kungia kwenye sekta hii. Wanajiuliza: je, ni wapi watapata
fedha?
“Ukosefu wa fedha wa kuanzisha
biashara” umeelezwa kuwa dalili mbaya ya tatizo linalozuia maendeleo ya wajasiriamali. Unahitajika ufumbuzi wa haraka ili kumkomboa mfanyabiashara mdogo.
Wakati mwingine tatizo
la upatikanaji wa mitaji unasababishwa na mabenki kukosa Sera za ukopeshaji zitakazowanufaisha
wafanyabiashara wadogo kwa kuweka masharti magumu yasiyotekelezeka. Kwa mfano:
· Kiasi cha juu cha kukopesha huwa ni kidogo sana kuweza kukidhi mahitaji;
· Mikopo hutolewa mijini tu, na kuacha sehemu
kubwa ya wananchi wanaoishi vijijini kukosa fursa hii
· Maombi ya mkopo huambatana na taratibu ngumu
kama kuwa na Leseni za biashara, TIN namba kutoka TRA n.k (Mfano: Muuzaji wa genge hana elimu ya Kodi hivyo
haoni sababu ya kuwa na vitu hivyo).
Pia Ukosekanaji
wa Vitambulisho vya kitaifa (Inawia vigumu kwa Mabenki kumtafuta mkopaji).
Mabenki na Wakopeshaji wanasemaje?
Kwa upande wa Mabenki na wakopeshaji nao
wanajitetea kuwa sio rahisi kutoa mkopo kwa mjasiriamali mdogo kutokana na
sababu zifuatazo:-
· Hurka wa watanzania katika kukwepa kulipa madeni
· Wajasiriamali wengi kukosa ofisi za kudumu na
zinazotambulika kisheria
· Upungufu uliopo kwenye sheria ya nchi unaomlinda
zaidi mkopaji aliyeshindwa kulipa deni na “kutomjali’ mkopaji
· Wajasiriamali kukosa dhamana zenye kutambulika
(mfano; mali zisizohamishika kama Hati za nyumba zilizosajiliwa).
· Ukosefu wa elimu ya utunzaji wa mahesabu
· Wajasiriamali wanakosa miradi ya maendeleo
inayosababishwa na kokosa ujuzi wa kufanya michanganua ya biasharazao.
No comments:
Post a Comment