Karibuni Mjasiriamali Blog


Karibuni tujumuike pamoja kupata habari za Kiuchumi na Ujasiliamali hususani katika sekta wa wafanya biashara wadogo wadogo sana (Micro business) katika kutoa elimu ya Ujasiriamali (Entrepreneurial skills) nchini Tanzania.
Hakika kuelimishana au kukumbushana mambo mbalimbali juu ya ujasiriamali hapa Tanzania kutaweza kutusaidia kuongeza ujuzi na kuongeza ufanisi wa biashara na kutoa fursa kwa wajasiliamali wapya kufahamu "ABC" za sekta hii muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yetu.

Nia ni kutoa maelezo kwa ufupi kuhusiana na dhana ya ujasiriamali, matokeo mazuri ya kutoa elimu ya ujasiriamali kama vile kukuza biashara; kuongeza kipato na kupunguza umaskini katika jamii ya mtanzania; na kuongeza mapato ya Serikali kwa ujumla.

Wajasiriamali wengi wanahitaji elimu katika mambo yafuatayo:-
  • Ufahamu wa mikakati ya mbinu za kukuza biashara;
  • Kujua mikakati ya kukabiliana na ushindani wamasoko;
  • Uelewa wa namna ya kumjali na kuvuta wateja; na
  • Ufahamu wa jinsi ya kuandaa na kutunza kumbukumbu za biashara zao.



2 comments:

  1. Wajasiriamali wengi hufeli kwenye kutofautisha matumizi yao binafsi,kimsingi biashara yako haihusiani na wewe ukilijua hili na ukatambua kuwa wewe pale ni kama mfanyakazi ndipo utapoweza kupiga hatua

    ReplyDelete