Katika pitapita za
blog hii ilikutana na tangazo ndani ya basi la daladala iliyokuwa imeandikwa “hata mbuyu ulianza kama mchicha” ni
kweli hata wazee walikuwa watoto. Na ni ukweli usiopingika kuwa biashara kubwa
kubwa tunazozishuhudia hazijashushwa kwa njia za mazingaombwe.
Wafanya biashara
maarufu kila mmoja ana historia iliyomfikisha katika mafanikio aliyofikia.
Reginald Mengi, Mohamed Dewji, na wengine wengi hawakuoteshwa kuwa na mafanikio
waliyonayo, bila kuwa na mwanzo uliowafikisha hapo walipo.
Fursa na mawazo mbalimbali
ya biashara yanatoka katika mazingira yanayotuzunguka; majumbani, makazini,
mashuleni, safarini n.k Wajasiriamali
waliofanikiwa hupata mawazo ya kuanzisha biashara, kuwa makini na kulifanyia
kazi wazo la biashara alilolivumbua katika mazingira yanayomzunguka.
Ni vema ukatoka nje
kujichanganya na watu ili uone fursa mbalimbali zilizopo kwa muda huo ambazo
zitaweza kukusaidia ukatoa maamuzi ya kuanzisha biashara yako huku ukikutana na
wafanyabiashara waliotangulia kwa kuiga tabia za kisiriamali. Kuna usemi usemao
“mvumbuzi sio tu kufumbua kitu bali ni
uchakarikaji wa kutafuta fursa na mawazo sahihi ya kuanzishisha biashara”.
Njia 3 za kuvumbua wazo sahihi la
biashara
Kwa kujifunza
kupitia kwa wengine wanaotuzunguka, utakutana na mawazo mbalimbali na ndio njia
ya kupata majibu ya kukuwezesha kujua ni biashara gani uanzishe. Kuna njia tatu
za kufuata:-
1.
Weka orodha ya mawazo yako
Hakuna biashara
isiyolipa; utashangaa mtu mmoja anafungua biashara leo inakufa baada ya miezi
sita. Lakini jirani yake ndani ya miezi sita anafungua na biashara nyingine ama
kupanua maradufu biashara yake. Kila siku ongeza angalau fursa moja kwenye
daftari lako. Usichague fursa; zote ni nzuri kama ukiwa na mipango na malengo.
Usikate tama,
jiulize kwa nini hawa wameweza na kwa nini wewe ushindwe? Jipe moyo “hashindwi
mtu hapa” Uhondo wa ngoma uingie ucheze mwenyewe. Na mara nyingine matatizo
ndio hupelekea mtu kujikuta anaangukia kupata wazo sahihi la biashara.
2.
Toka nje, jichanganye na watu
Mawazo ya
kibiashara hayapatikani kwa kukaa ndani na kusubiri wazo lishuke kutoka mbinguni.
Unahitajika ubunifu ambao unaweza kuupata kupitia maonyesho ya biashara,
kutembelea wafanyabiashara wazoefu na kubadilishana mawazo. Ikiwezekana “wawinde”
wafanyabiashara unaowafahamu ambao unaweza kuongea kuhusu wazo lako. Ishi kwa
kuangalia wanavyoendesha biashara zao. Wengi hukatisha watu tama, usiwajali.
3. Iga mbinu za kupambana na changamoto
Matatizo yapo kila
siku, kila sehemu, muda wowote. Biashara zote zina changamoto, jifunze ni jinsi
gani wafanyabiashara wanavyopambana na changamoto zinazowazunguka na utapata
njia muafaka ya kupambana na hivyo kuendelea na maisha. Iga na uweze kuzitumia
mbinu hizo ila kuwa makini kiga mazuri huku ukiyaacha yale mabaya.
Kweli kabisa kila kitu kina mwanzo na vingine vilianza vidogo sana
ReplyDeletekila siku napata nafasi ya kujua mambo mapya juu ya taaluma hii muhimu ya kupambana na changamoto zinazo ikabili jamii, hongeleni na endeleen kuandika habari juu ya taaluma hii muhimu
ReplyDeleteNazid kujfunz mambo mengi na mhim xn ktk maisha yangu kuptia kwenu, hongern xn na Mungu was mbingun awabark!
ReplyDelete